qurani tukufu

IQNA

IQNA – Mamlaka ya Fatwa ya Misri (Dar al‑Ifta) imetangaza kwamba matumizi ya programu za akili mnemba (AI), ikiwemo ChatGPT, katika kufasiri Qur’ani Tukufu hayaruhusiwi kisheria.
Habari ID: 3481861    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/28

IQNA – Akilaani matukio ya hivi karibuni ya kuvunjiwa heshima Qur’ani Tukufu, mwanaharakati wa Qur’ani kutoka Iran ametoa wito wa kuundwa kwa Jumuiya ya Kimataifa wa Maqari wa Qur’ani ambayo miongoni mwa majukumu yake ni kufuatilia hatua za kisheria dhidi ya vitendo hivyo.
Habari ID: 3481856    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/27

IQNA-Mashindano ya Qur’ani kwa wasichana yamefanyika katika mkoa wa Hajjah nchini Yemen, yakionyesha juhudi za kuimarisha elimu ya Qur’ani miongoni mwa wanafunzi wa kike.
Habari ID: 3481855    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/27

IQNA – Waziri wa Mambo ya Dini na Awqaf wa Algeria amewakabidhi wanazuoni wa Afrika nakala ya kihistoria ya Qur'ani Tukufu ijulikanayo kama “Rhodosi”, wakati wa kongamano lililofanyika nchini humo kuhusu diplomasia ya kidini.
Habari ID: 3481851    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/26

IQNA – Nakala 114 adimu za Qur'ani Tukufu kutoka nchi 44 zimewekwa katika maonyesho maalumu yanayofanyika mjini Istanbul, Uturuki.
Habari ID: 3481850    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/26

IQNA – Jumuiya ya Watumishi wa Qur’ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani machafuko ya hivi karibuni yaliyoungwa mkono na tawala zakigeni, na ikalisifu taifa la Iran kwa kuvuruga njama za maadui.
Habari ID: 3481849    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/26

IQNA – Ensaiklopidia Maalumu ya Usomaji wa Qur’ani na Sayansi Zake imezinduliwa na Qatar kama kazi mpya inayolinda uhalisia wa kielimu huku ikileta urithi wa qira’ah katika muundo wa kidijitali kwa watafiti na wapenda taaluma za Qur’ani.
Habari ID: 3481848    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/26

IQNA – Toleo la pili la mkutano wa kimataifa kuhusu “Tafsiri ya Qur’ani na Akili Mnemba” linatarajiwa kufanyika nchini Morocco.
Habari ID: 3481845    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/25

IQNA – Nakala ya kihistoria na yenye thamani kubwa ya Qur'ani Tukufu, inayojulikana kama “Qur'ani ya Kufi,” imewekwa wazi kwa umma katika Makumbusho ya Qurani ya Makka.
Habari ID: 3481840    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/24

IQNA – Aplikesheni mahiri ya “Al Moeen” imezinduliwa katika hafla maalumu iliyofanyika Alhamisi katika Chuo cha Qur’ani Tukufu mjini Sharjah, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Habari ID: 3481837    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/23

IQNA-Hafla ya kuanza kurekodi qiraa au usomaji wa Qur’ani Tukufu kwa mtindo wa tartīl kwa riwaya za Warsh na Qālūn imefanyika katika Redio ya Mauritania.
Habari ID: 3481831    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/21

IQNA – Kikao cha usomaji wa Qurani kimefanyika katika Msikiti wa Hazrat Abulfadh (AS) mjini Ahvaz, kusini magharibi mwa Iran, tarehe 19 Januari 2026, kwa mnasaba wa Eid al-Mab’ath, siku ya kukumbuka kutumwa kwa Muhammad (SAW) kuwa Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu.
Habari ID: 3481826    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/20

IQNA – Maonyesho yenye kichwa “Shahidi wa Qur’ani” yameandaliwa katika mkoa wa al-Hudaydah, Yemen, yakitoa heshima kwa Sayyid Hussein Badreddin al-Houthi, ambaye nchini humo anajulikana kama shahidi wa Qur’ani.
Habari ID: 3481815    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/18

IQNA – Kitivo cha Lugha cha Chuo Kikuu cha Al-Azhar nchini Misri kinaendeleza mradi mahsusi wa tafsiri na tarjuma unaolenga kuufikisha ujumbe wa Qur’ani Tukufu kwa mataifa mbalimbali duniani.
Habari ID: 3481798    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/13

IQNA – Jumuiya ya Qur’ani ya Iran imelaani vikali machafuko mabaya yaliyotokea hivi karibuni nchini. Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, jumuiya hiyo iliwashukuru vikosi vya ulinzi na usalama kwa juhudi zao za kurejesha utulivu na amani katika jamii.
Habari ID: 3481793    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/12

IQNA-Kongamano la pili la Siku ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu limefanyika Jumapili 11 Februari jijini Qum, Iran, sambamba na kukaribia tarehe 27 Rajab ambayo inatambuliwa kama Siku ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ukumbi wa Bibi Fatima al‑Ma‘suma (SA.)
Habari ID: 3481791    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/12

IQNA – Kifaa kipya cha kielektroniki cha eBraille kilichotengenezwa nchini Malaysia kimeleta mageuzi makubwa katika kujifunza Qur'ani Tukufu kwa watu wenye uoni hafifu, au ulemavu wa macho kwa kuwapa uwezo wa kupata maandiko ya dini moja kwa moja kwa njia ambayo haijawahi kupatikana hapo awali, sambamba na kufungua fursa katika nyanja nyingine za elimu.
Habari ID: 3481789    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/11

IQNA – Msimamizi mkuu wa mashindano ya vipaji vya Qur’ani nchini Misri, maarufu kwa jina “Dawlat al-Tilawa”, ametangaza kuwa msimu mpya wa kipindi hicho kitaanza rasmi Novemba 2026.
Habari ID: 3481784    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/08

IQNA – Mwana wa qari maarufu wa Misri aliyefariki, Abdul Basit Abdul Samad, amepongeza kuanzishwa kwa Jumba la Makumbusho la Waqari wa Qur’an nchini humo.
Habari ID: 3481782    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/08

IQNA – Kiwanda cha Mfalme Fahd cha Kuchapisha Qur’an kilichoko mjini Madina, Saudi Arabia, kilipokea wageni wapatao milioni moja kutoka ndani na nje ya nchi mwaka uliopita.
Habari ID: 3481779    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/07